Sunday, May 15, 2011


RAIS MISS UMOJA WA MATAIFA KUTUA TANZANIA MWEZI UJAO



Baada ya Tanzania kwa mara ya kwanza kuwa wenyeji wa shindano la Dunia la urembo miaka mitano iliyopita, shindano la Miss Tourism World 2006 lililo fanyika katika ukumbi wa Ubungo Plaza 11-3-2006, Kupitia Miss Tourism Tanzania Organisation ,waandaaji wa mashindano ya Miss Utalii Tanzania, Tanzania imepewa heshima tena ya kuwa wenyeji wa shindano jingine la Dunia, safari hii ikiwa ni shindano la Miss Umoja wa Mataifa 2011 (Miss United Nation 2011), ambalo limepangwa kufanyika nchini mwezi Disemba 2011 mwezi ambao Tanzania itakuwa inaadhimisha miaka 50 ya uhuru. Shindano hilo litashirikisha nchi 120 kutoka duniani kote na litaonyeshwa moja kwa moja toka Tanzania katika Televisheni mbalimbali Duniani kote.
Akithibitisha habari hizo, Rais wa Miss Utalii Tanzania, Erasto Gideon Chipungahelo, alisema kuwa mkataba wa awali umekwisha sainiwa na waandaaji hao wa Miss Umoja wa Mataifa,na taratibu za kufanyika kwa shindano hilo nchini zinaendelea, ikiwemo kutoa Taarifa Serikalini kupitia Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ,ambayo ni Mamlaka ya Serikali ya kusimamia Sanaa na Burudani nchini.
Aidha Chipungahelo, alithibitisha kuwa Rais wa Dunia wa Miss Umoja wa Mataifa Neville Wiliams,akiambatana na ujumbe wa kamati ya Dunia ya mashindano hayo anatarajiwa kuwasili nchini mwishoni mwa mwezi wa sita mwaka huu, katika Ziara ya ukaguzi na kukamilisha taratibu husika ikiwemo kufanya mkutano wa kimataifa wa waandishi wa habari . Akiwa nchini atafanya mikutano na viongozi mbalimbali wa mamlaka za Serikali, makampuni binafsi na mashirika ya umma ambayo yanaweza kudhamini fainali hizo za dunia. Pia watakutana na kukagua vituo mbalimbali vya Televisheni nchini, ili kupata kituo cha Televisheni kitakacho shirikiana na vituo vya nje kurusha na kusambaza Matangazo ya moja kwa moja ya fainali hizo kutokea Tanzania.
Wakati wa fainali hizo, pamoja na warembo 120,wanatarajiwa kuambatana na  wakurugenzi wao wa  taifa 120, waandishi wa habari kutoka katika nchi zao 120,waandishi wa habari wa kimataifa 60,marafiki na wanafamilia wa washiriki 240,viongozi wa mashindano hayo 15 na wataalam wa mashindano hayo 30. Zaidi ya wageni 705 kutoka nje wanatarajiwa kuwako nchini kwa ajili ya shindano hilo, ambalo litaangaliwa moja kwa moja na zaidi ya watazamaji Bilioni 1 wa Televisheni na mitandao ya Tovuti duniani kote.
Hii itakuwa ni fulsa nyingine ya pekee kwa Tanzania kujitangaza kitalii, kiuchumi na kitamaduni, pia kuonyesha moja kwa moja mafanikio makubwa ya Tanzania katika miaka 50 baada ya uhuru, tulio upata mwaka 1961 kutoka wakoloni wa Uingereza.
Tunatoa mwito kwa makampuni ya Tanzania, na Watanzania kwa ujumla kujitokeza kudhamini fainali hizi za Dunia, ili kupata fulsa ya kujitangaza kimataifa na kuweza kupenyeza bidhaa na Huduma za Tanzania katika soko la kimataifa.
Tanzania katika fainali hizo itawakilishwa na Miss Utalii Tanzania 2011, Adelqueen Njozi.



MISS TOURISM TANZANIA ORGANISATION SASA TAASISI YA KIMATAIFA

Miss Tourism Tanzania Organisation,waandaaji wenye haki miliki ya shinadano la Miss Utalii Tanzania,sasa waimingia katika kundi la taasisi za kimataifa za kutangaza na kupromoti Utalii na utamaduni.Hii nibaada ya kuwa taasisi ya kwanza nchini kumiliki mashindano ya Dunia ya Utalii ya urembo,riadha,mpira wa ufukweni,Safari za Kimataifa za Utalii na maonyesho ya kimataifa ya Utalii ya Mavazi. Mashindano hayo ni Miss Utalii Vyuo Vikuu Dunia ( Miss Tourism University World),Miss Urithi wa Dunia ( Miss Heritage World),Mbio za Kimataifa za Nyika za Hifadhi za Taifa (National Parks International Marathon),Safari kuu ya Kitalii Tanzania ( Tanzania Great Safari & Tour), Maonyesho ya kimataifa ya Mavazi ya Kitalii (Tanzania Great Safari Fashion Show) na Miss Tourism Beach Soccer